Open top menu

Wasanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh Kiba ‘Aki Kiba’ kesho Jumapili wanatarajiwa kutumbuiza katika uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Diamond na Ali Kiba ni sehemu ya wasanii wengi wa muziki na wale wa filamu watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Kitendo cha Ali Kiba na Diamond kupanda jukwaa moja ni nadra kutokea kutokana na upinzani uliopo kati yao, hiyo watu watakaofika kwenye uzinduzi huo watapata burudani ya bure ya aina yake.

Written by zipsuit

Newer Post
This is the last post.

.

.